MUWEKEZAJI IRAD KUANZA MATENGENEZO YA BARABARA YA KM. 12 MLIMBA-KILOMBERO


Kampuni ya IRAD inayojishughulisha na kilimo cha mazao ya viungo vya chakula katika kijiji cha TAWETA Kata ya Masagati katika Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero ameanza matengenezo ya barabara ya Pumbwe-IRAD-Kitete pamoja na ujenzi wa madaraja.

Timu ya IRAD pamoja na TARURA ikiongozwa na Meneja wa TARURA Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Ndyamukama imetembelea  mradi huo na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya kuboresha matengenezo hayo pamoja na kuanza taratibu za usajili wa barabara. 

Kukamilika kwa barabara hiyo  yenye urefu wa Km. 12 itafungua mawasiliano kati ya Kata ya Masagati-Mlimba na Mkoa jirani wa Njombe pia itawasaidia wananchi kusafirisha mazao yao.

Post a Comment

Previous Post Next Post