TUIKATAE PROPAGANDA YA "KUJITEKA" INAYOENEZWA NA WAFUASI WA POLEPOLE


Tukio la Humphrey Polepole "kujiteka" limeelezwa na wachambuzi wa siasa na usalama kama dhihirisho na mfano halisi wa namna ambavyo Propaganda inavyoweza kutengenezwa, kupangwa na kuaminishwa kwa umma kupitia mchanganyiko wa hisia za hofu, huruma na udhabiti wa simulizi.


"Katika dunia ya siasa za kisasa, ukweli hauuzwi; hisia ndizo bidhaa kuu. Wananchi wanapaswa kuwa na umakini mkubwa kutenganisha ukweli wa kisiasa na michezo ya propaganda." Anasema George Orwell katika chapisho lake la 'udanganyifu wa kiulimwengu, kusema ukweli ni tendo la mapinduzi.'


Katika mazingira ya kisiasa ya Tanzania, simulizi huwa na nguvu kuliko ukweli na tukio la hivi karibuni la madai ya kutekwa kwa mwanasiasa Humphrey polepole, akidaiwa kutekwa na watu wasiojulikana limezua gumzo kubwa. Ni bahati mbaya kwamba badala ya wengi kulitazama tukio hili kama tukio la kihalifu, Mchambuzi Michael Douglass Mwansansu anasema tukio hilo ni mkakati uliopangwa kwa ustadi ili kujenga taswira mpya ya kisiasa.


"Katika muktadha wa "kujiteka" propaganda inatumiwa kuunda simulizi la mwanasiasa mnyonge anayepigania haki. Hii ni mbinu ya self Victimization ambapo mwanasiasa hujenga huruma ya umma kwa kuonekana mwathirika wa njama za kisiasa na hata watu wanaodai kuwa Polisi ndio wamefanya vile tujiulize imekuaje wamkamate waache vifaa kama Laptop na vinginevyo pamoja na simu zake?" Amehoji Mwansasu.

Kulingana na Mwansasu, katika muktadha huo wa kujiteka taarifa huandikwa kwa maneno ya uchungu, machozi na maneno kama 'tulijaribu kumtafuta bila mafanikio', suala ambalo huamsha huruma za wananchi na kuibua hisia dhidi ya maadui wa kisiasa.

Kulingana na mchambuzi huyo, Propaganda ya Polepole kama zilivyo propaganda nyingine huitaji adui ambaoo kupitia madai haya ya utekaji, simulizi hujenga picha ya kundi lisilo na utu linalopambana na mwanasiasa mzalendo, suala ambalo amelitaja kama silaha ya kuimarisha umoja wa wafuasi wa muhusika wa propaganda.

Akizungumzia athari za propaganda kwa jamii, Mwansasu amesema propaganda kama hii ya Polepole huathiri imani ya wananchi kwa taasisi na inapovutia hisia wananchi hufanya maamuzi ya kisiasa kwa msingi wa huruma badala ya hoja, huku vyombo vya habari visivyokuwa makini vikipotoka na kueneza simulizi hizo bila uchambuzi na hivyo kuimarisha uongo uliofichwa kwa mantiki ya usalama wa Taifa.

Aidha Mwansasu anaeleza kuwa tukio kama la 'kujiteka kwa Polepole'ni muhimu likatazamwa kupitia nadharia ya kuunda ajenda (Agenda setting) ambapo vyombo vya habari havisemi watu wafikirie nini bali vinawaelekeza wafikirie kuhusu nini, akisema kupitia kuikuza propaganda hiyo umma unageuzwa kutoka kujadili hoja za sera na kuelekezwa kwenye huruma na taharuki na hatimae kubadili mwelekeo wa mazungumzo ya kisiasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post