Isaya Mwakajana, Kijana Mbunifu wa Maudhui, Mpiga Picha Mahiri na Mwandishi wa habari nchini Tanzania, amesisitiza umuhimu wa jamii
kuthamini ubunifu kama chachu muhimu ya kujikwamua kiuchumi kwa vijana.
Kauli hii imetolewa wakati wa warsha ya vijana na uchumi “Vijana Think Tank” iliyofanyika Jijini, Dodoma wiki hii.
Isaya Mwakajana, ambaye ni muandaaji wa maudhui ya picha, sauti na video pia na mchambuzi wa masuala ya siasa, aliweka msisitizo juu ya jukumu la ubunifu katika kuleta maendeleo endelevu. Alisisitiza kuwa vijana wanaweza
kuwa na nguvu ya kubadilisha jamii na kuchangia ukuaji wa kiuchumi kupitia ubunifu wao.
"Tunapaswa kutambua na kuthamini vipaji vya vijana wetu ubunifu si tu katika sanaa au teknolojia bali pia katika maeneo yote ya maisha, vijana wanaweza kuleta mabadiliko makubwa kama jamii itawapa nafasi na msaada unaohitajika," alisema Isaya Mwakajana Lalika.
Akiangazia changamoto zinazowakabili vijana hasa katika upatikanaji wa ajira,Mwakajana aliweka bayana kuwa kuhamasisha ubunifu kutawawezesha vijana wengi kugundua fursa mpya za kiuchumi, hivyo sasa jamii tuanze kutengeneza mazingira rafiki na kuwekeza katika programu zinazosaidia kuendeleza vipaji
vya vijana.
Warsha hiyo ya Vijana Think Tank ilijumuisha mijadala na mifano halisi ya vijana waliofanikiwa kutumia ubunifu wao kujenga kazi na biashara
zinazolenga kuboresha maisha yao na jamii kwa ujumla, Mwakajana aliwahimiza vijana waendelee kushiriki na kujifunza ili kufanya mabadiliko
chanya yanayohitajika katika mtazamo wa jamii kuhusu ubunifu.
Kwa kumalizia, Isaya Mwakajana aliwahimiza vijana kujiamini na kutokata tamaa pia, akasisitiza kuwa ubunifu na kujituma na njia mojawapo inayowezakukupa mafanikio wakati wowote, kauli hii ilifungua dira mpya kwa washiriki wa warsha hiyo ya Vijana Think Tank kwa kupata matumaini ya kuona jamii inayothamini na kuunga mkono ubunifu wa vijana kama nguvu ya kuleta
mabadiliko chanya kiuchumi