MHE. ENOCK KOOLA AAHIDI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO WANAOJITOLEA SHULE YA SEKONDARI DARAJANI


Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo MHE. ENOCK KOOLA ametembelea rasmi Shule ya Sekondari Darajani, ambapo alikutana na wadau wamaendeleo waliowahi kusoma shuleni hapo ambao wamekuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya Shule hiyo.

Mheshimiwa Mbunge amekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika Jimbo la Vunjo. 

Kutokana na mchango wake wa muda mrefu, amekuwa akishirikishwa mara kwa mara katika shughuli za maendeleo ya shule hiyo. Mwezi Desemba, alialikwa kushiriki harambee ya Alumni iliyolenga kuchangisha shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha maabara ya kisasa ya TEHAMA (Computer Laboratory).

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Mbunge alipata fursa ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Alumni, ikiwemo:

Kubadilisha madirisha yote ya nyavu na kuweka madirisha ya kisasa ya vioo

Kufunga miundombinu mipya ya umeme katika shule nzima Kuleta madawati na kompyuta za kisasa

Kujenga majengo mapya na kufanya ukarabati wa ofisi ya Mkuu wa Shule Kuweka paving blocks kwenye njia zote za kutembea

Kujenga vyoo vya kisasa zaidi ya matundu nane vyenye vioo, masinki ya kisasa ya terrazzo na mfumo wa maji wa kisasa

Mheshimiwa Mbunge amepongeza juhudi za Alumni na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuinua sekta ya elimu na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Darajani.

Post a Comment

Previous Post Next Post