AFISA TARAFA KATERERO AFIKA KATA KWA KATA KUSHIRIKI VIKAO VYA KUTOA ELIMU KUHUSU MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE


Wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Rais Samia Suluhu Hassan aliahidi endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atakuja na Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata Bima itakayowasaidia kupata matibabu popote nchi nzima bila changamoto yoyote ile.

Serikali ya Rais Samia inatimiza ahadi hii na sasa inatoa elimu kwa wananchi, viongozi mbalimbali wa Kata, Vijiji, Vitongoji, viongozi wa dini na kijamii n.k kuelekea kuanza kwa Mpango huu wa Bima ya Afya kwa Wote.

Wiki hii kuanzia Januari 6, 2026 hadi leo Alhamisi, Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku akiongozana na Wataalamu wa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba ameendelea kushiriki vikao mbalimbali kwenye Kata mbalimbali ndani ya Tarafa ya Katerero vya kuwajengea uwezo viongozi na watumishi wa umma kujua kiundani Mpango huu wa Serikali wa Bima ya Afya kwa Wote na namna unavyokwenda kutekelezwa ili na wao wakatoe elimu hiyo kwa wananchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post