Timu ya wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E) ya Wizara ya Maliasili na Utalii imekutana katika kikao cha robo mwaka kwa lengo la kuweka mikakati ya utekelezaji wa majukumu ya Idara na vitengo vya wizara hiyo kwa wakati.
jAidha, Bi. Nassibu amesema kuwa Kitengo anachokiongoza kimejipanga katika kuhakikisha kuwa Ufuatiliaji na Tathmini ya majukumu na miradi ya Wizara unaleta matokeo tarajiwa na kutoa matokeo kwa wadau mbalimbali ili wafahamu namna Wizara hiyo ilivyotekeleza majukumu yake kwa maslahi ya Watanzania wote na kwa sekta ya Uhifadhi na Utalii kwa ujumla.
Kikao kazi hizo chenye wajumbe kutoka taasisi (Wakuu wa Vitengo vya M&E) na M&E Champions wa idara na vitengo vya Wizara hiyo, pamoja namambo mengine, wajumbe hao wataandaa taarifa ya utendaji wa Wizara kwa Julai - Desemba 2025 na kitahitimishwa kwa ziara ya kutembelea shughuli za TAWA jijini Dodoma.
