Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko ametaka mpango mkakati wa kuiwezesha Tanzania kuweza kufikia uchumi wa kiwango cha kati cha juu ili kuondokana na changamoto ya kusalia kwenye kiwango hicho kwa muda mrefu.
Akizungumza wakati wa kongamano la Kikanda la kukusanya maoni kuhusu dira ya maendeleo ya mwaka 2050, Amesema ni muhimu kubadili mfumo uliopo na kutia bidii katika kukuza uchumi wa nchi kupitia maoni na maono ya watanzania katika ujenzi wa Tanzania ya miaka 25 ijayo.
Amesisitiza umuhimu wa kujiuliza kuhusu aina ya Mtanzania anayehitajika kwenye mipango ya nchi miaka 25 ijayo, jamii inayotakiwa ili kusaidia katika kufikiwa kwa malengo na mipango inayopangwa kwenye dira hiyo ya maendeleo ya miaka 25 ijayo.