WASIRA: BADALA YA KULALAMIKA FANYENI KAZI MUWE KAMA SAMIA.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amewataka watu wanaohoji kwanini wanamsifia Mwenyekiti wa chama hicho Samia Suluhu Hassan kuacha kulalamika badala yake nao wafanye mambo mazuri ya maendeleo ili wasifiwe.

Akizungumza mjini Musoma leo Septemba 6,2025 kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Musoma Mjini, lenye kata 16 ambapo kata mbili kati ya hizo wagombea udiwani wa chama hicho wamekosa wapinzani.

Ndg. Wasira amewataka watu wanaohoji kwanini wanamsifia Mwenyekiti wa chama hicho Samia Suluhu Hassan kuacha kulalamika badala yake nao wafanye mambo mazuri ya maendeleo ili wasifiwe.

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake Rais Samia amefanya mambo makubwa  ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za kijamii ikiwemo katika sekta za afya,maji, elimu na sekta zingine na kwamba chama chake bado kinalenga kufanya mambo mengine makubwa kwa wananchi.

Wasira amesema lengo la chama hicho ni kuendelea kushika dola ili kuwatumikia wananchi na ndio maana wameandaa ilani bora yenye kujibu mahitaji na changamoto zete za wananchi. 

"Sasa wanalalmika nini wakati hawana chochote walichokifanya,sisi lazima tumsifie wa kwetu kwasababu amefanya mengi sana na tunayaona,sasa wewe unalalamika wakati hata zahanati haujajenga,fanya maendeleo na wewe usifiwe kwasasa tuko na mama Samia," amesema.

Wasira amesema chama hicho kina malengo mazuri na wananchi na ndio maana kimerudi tena kuomba ridhaa ya kushika dola huku akisema katika jimbo la Musoma mjini na mkoa mzima wa Mara yapo mengi mazuri yaliyopangwa kufanyika kwa maslahi ya wakazi wa jimbo hilo

Post a Comment

Previous Post Next Post