WANANCHI WA KUTEMBE-MWALONI MULEBA WAONDOKANA NA ADHA YA BARABARA


Ujenzi wa barabara ya lami ya Katembe -Mwaloni inayounganisha Barabara kuu ya kutoka nchi za Uganda, Rwanda na Burundi katika wilaya ya Muleba  Mkoani Kagera  uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 400 umeleta ahueni kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na wafanyabiashara wa samaki kutoka katika visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria kwenda ndani na nje ya Nchi.

Kiongozi wa mbio za Mwenge  wa uhuru Kitaifa Ndugu Ismail  Ussi ameridhisha na viwango vya mradi huo na kuwapongeza TARURA kwa utekelezaji wa mradi wenye viwango ambao unaendeleaa kuwasaidia wananchi .

Alisema kuwa Ili wanachi wapate huduma bora na nguvu ya kuzalisha wanahitaji Barabara nzuri zenye viwango na kupitia umma wa wananchi ameshukuru usimamizi wa mradi huo na namna Halmashauri ya Muleba ulivyotoa mapato ya ndani kujenga Barabara imara inayoweza  kuchochea uchumi na kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nje ya nchi .

Meneja wa TARURA wilaya ya Muleba  Mhandisi Dativa Semforiani  akitoa  taarifa ya mradi wa Barabara  ya Katembe-Mwaloni amesema uwepo wa barabara hiyo imekuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na kuongeza pato la halmashauri ya wilaya ya Muleba.

Alisema barabara iliyozinduliwa ni ya kwa kiwango cha lami ni Km 0.5 ambapo Barabara hiyo ni kiunganishi kikuu Cha wananchi wa eneo hilo na wafanyabiashara wa Rwanda ,Burundi Uganda na Congo hasa wale wanaonunua mazao ya dagaa na samaki 

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kumeibua hisia za tabasamu kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambapo baadhi ya wakazi wa eneo la Mwaroni na wafanyabiashara wamesema kuwa awali kabla ya ujenzi wa barabara hiyo nyakati za mvua samaki zao ziliharibika kutokana na ukosefu wa magari ya kusomba mizigo kwenda sokoni na hivyo kusababisha hasara.

Post a Comment

Previous Post Next Post