NYUMBA KWA NYUMBA, KIJIJI KWA KIJIJI KATA YA BUPU -MKURANGA


Leo tar 08/09/2025  Mgombea Ubunge wa mkuranga ndugu @abdallahulega ameanza rasmi kampeni zake za kutembelea kata, vijiji na vitongoji vya jimbo la mkuranga.

Mapema asubuhi ya leo ameanza na kata ya Bupu kwa kuwatembelea wananchi na makundi mbalimbali wakiwemo, wafanya biashara wadogo, maafisa usafirishaji maarufu boda boda kwenye migundi yao mbalimbali pamoja na kushiriki shunghuli na michezo mbalimbali.

Aidha mh @ulega ameeleza mambo makubwa na ya msingi ambayo ameyatekeleza kwenye Nyanja zote za maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya uhakika na ambayo ilikuwa kero kwa wanachi wa bupu, ujenzi wa zahanati, ujenzi wa shule na madarasa kwa ngazi zote msingi na sekondari, pia upatikanaji wa maji safi na salama pamoja kusogezwa kwa huduma ya umeme vyenye vitongoji vingi vya kata ya Bupu.

Pia ndugu @abdallahulega ameeleza kwa urefu na mapana na kutoa ahadi kwa wananchi wa kata ya Bupu, ikiwemo uendelezaji juhudi za utekelezaji wa mipango ya  maendeleo zaidi, kwenye nyanja zote ikiwemo Elimu- ikihusisha ngazi msingi na sekondari, Afya, Umeme, Maji safi na salama, na miundombinu na mtandao wa Barabara zinazounganisha Kata ya Bupu. 

Mwisho, ndugu @abdallahulega amemuombea kura nyingi na za kishindo Mh Rais @samia kwa wanachi wa kata ya Bupu kwa kuwa ndio shujaa na kiongozi pekee aliyeleta miradi mingi ya  maendeleo kwenye kata hio tangu aingie kwenye awamu yake ya uongozi.

Post a Comment

Previous Post Next Post