Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Dkt. Mwl. Haroun Ali Suleiman amepongeza ushirikiano wa watendaji wa Wizara yake na Wizara ya Katiba na Sheria (Bara) katika kufanikisha utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kwa Zanzibar.
Mhe. Dkt. Mwl. Suleiman ameyasema hayo leo tarehe 10 Mei 2025 wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo kwa mkoa wa Kusini Unguja ambapo mgeni rasmi alikua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Amesema wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma za Msaada wa Kisheria ambazo zimewafikia na zitatolewa bila malipo ili waweze kutatuliwa kero zao.