HUDUMA ZA KIJAMII ZIMEBORESHWA ZAIDI KWA MIAKA 25 ILIYOPITA"- PROF. KITILA MKUMBO.


Huduma za kijamii nchini Tanzania ikiwemo huduma za afya, elimu, maji na umeme ni miongoni mwa huduma zilizoimarika zaidi na kukua kwa kasi kufuatia utekelezaji wa dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 inayotekelezwa mpaka mwaka 2025/2026.

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais- Mipango na uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo ametaja huduma hizo kuwa ni pamoja na huduma ya maji ambapo mwaka 2000, mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa dira ya mwaka 2025 huduma hiyo ilipatikana kwa asilimia 32% pekee kwenye maeneo ya vijijini na kufikia mwaka 2022, huduma hiyo imepatikana kwa 77% kwenye vijiji vya Tanzania.

Waziri Prof. Kitila pia amesema mwaka 2000 ni kaya 10% tu ndizo zilizokuwa zinapata huduma ya umeme nchini Tanzania na kufikia mwaka 2022 serikali imefanikiwa kufikisha huduma ya umeme kwenye zaidi ya kaya 77%.

Akizungumzia huduma ya elimu, Waziri Prof. Kitila amesema mwaka 2000 kati ya watoto 100 waliokuwa wanamaliza elimu ya msingi ni 10% pekee waliokuwa wanapata fursa ya kuendelea na masomo ya sekondari kutokana na sababu mbalimbali ambapo kwasasa asilimia hiyo imeongezeka na kufikia 70% huku lengo likiwa ni kufikia 90% mwaka 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Mipango na uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo alikuwa akizungumza kwenye kongamano la Kikanda, Kanda ya kusini yenye mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na Songwe, Kongamano lenye nia ya kukusanya maoni ya wananchi kwenye uandishi wa Dira mpya ya ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2025- 2050.

Post a Comment

Previous Post Next Post