DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO NI YA WANANCHI"- MTANDA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema kufanyika kwa kongamano la Kikanda la maandalizi ya dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050, ni fursa nzuri katika kuangazia shughuli zinazofanywa na wananchi na kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa changamoto zinazowakabili kwenye ustawi wao na shughuli zao za kiuchumi.

Mhe. Mtanda ametoa kauli hiyo leo Julai 20, 2024 wakati akiwakaribisha viongozi mbalimbali wa serikali wanaoongozwa na mgeni rasmi Dkt. Doto Biteko pamoja na wananchi mbalimbali kwenye Kongamano la kwanza la kikanda la maandalizi ya dira ya Taifa ya maendeleo.

Mhe. Mtanda amesisitiza kuwa dira ya maendeleo ni ya wananchi akisisitiza dhamira ya serikali katika kugusa maisha ya wananchi akiwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kama ishara ya uzalendo na shauku ya kushiriki kwenye mipango ya maendeleo ya Taifa.

Mtanda kadhalika ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoingozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye mkoa wa Mwanza ikiwemo ujenzi wa meli ya Mv. Mwanza yenye kugharimu takribani Bilioni 123, daraja la Kigongo-Busisi, reli ya kisasa ya SGR pamoja na miradi mbalimbali ya miundombinu ya vivuko, masoko na miradi ya maji katika Mkoa wa Mwanza.

Post a Comment

Previous Post Next Post