TANZANIA YATOA USHUHUDA WA MAFANIKIO UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI VIJIJINI


Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso Katika Mkutano wa Mawaziri wa Maji na Fedha wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika kuhusu huduma ya maji na usafi wa mazingira uliondaliwa na Benki ya Dunia Jijini Addis Abab, Ethiopia; ametoa ushuhuda wa mafanikio na uzoefu wa utekelezaji wa programu ya lipa kwa matokeo, PforR inayolenga utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijni.

Akizungumza katika Mkutano huo Waziri Aweso amesema siri ya mafanikio, Moja ni Utashi wa kisiasa na azma ya Mkuu wa nchi katika kuwaondolea adha ya maji wananchi waishio vijijini na hasa wanawake na watoto wa kike na hapa akitoa ushuhuda wa nia na dhamira ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika lengo la kumtua Mwanamama ndoo kichwani.

Pia, ameeleza juu ya Usimamizi thabiti na ufatiliaji wa karibu wa hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi, Ufanyaji kazi kwa bidii na kujituma miongoni mwa watendaji, Utoaji wa motisha kwa watendaji wanaofanya vizuri, uwazi na matumizi sahihi ya fedha na swala zima la ujenzi wa miradi bora yenye uendelevu.

Aidha, Kwa mujibu wa Benki ya Dunia Tanzania ndio kinara wa utekelezaji wa Program ya PforR kati ya nchi zaidi ya 50 zinazotekeleza mpango huu unaoratibiwa na Benki ya Dunia.

Mwisho, Kufuatia maombi ya nchi mbalimbali kuja Tanzania kujifunza utekelezaji wa Program hii, Mhe. Aweso amezikaribisha nchi mbalimbali Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post