NDEJEMBI:BIL.14.5/- ZA TACTIC KUJENGA MIUNDOMBINU MTWARA


Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe.  Deogratius Ndejembi amesema Serikali kupitia mradi wa kubadilisha miundombinu na ushindani wa miji nchini (TACTIC) imetenga Sh. Bilioni 14.5 kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha mabasi pamoja na barabara mbili zenye urefu wa kilometa sita katika Mkoa wa Mtwara.

Mhe.Ndejembi ametoa kauli hiyo leo kwenye ziara ya Naibu Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Doto Biteko mkoani Mtwara ambapo amesema kiasi hicho cha fedha pia kitawezesha kujengwa kwa karakana kwa ajili ya wajasiriamali wadogo.

"Mhe. Naibu Waziri Mkuu niwahakikishie wananchi wa Mtwara siyo tu Mtwara Manispaa ndio watanufaika na mradi huu wa TACTIC, mipango ya Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kuwa  Halmashauri tatu za Miji ya Nanyamba, Newala na Masasi pia zinanufaika kwa kupata fedha za mradi huu wa TACTIC."

"Maelekezo yangu kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ni kwa wahandisi washauri kuhakikisha hadi kufikia Desemba 10 mwaka huu wawe wamesaini mikataba ya michoro ya mradi kwenye halmashauri hizo," amesema Mhe. Ndejembi.

Aidha amesema bajeti ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) katika Mkoa wa Mtwara imepanda kutoka Sh. Bilioni saba kwa mwaka hadi Sh.Bilioni 23.8 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya barabara ndani ya mkoa huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post