Serikali haiwezi kuuza bandari na bandari haiuziki’

Ni Julai 29, 2023 ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo anazungumza na Wananchi kwenye Mkutano wa Chama ulioandaliwa Kawe Jijini Dar es Salaam huku akiongozana na viongozi mbalimbali wa Chama hicho.

Serikali haiwezi kuuza bandari na bandari haiuziki, huu ndiyo mkataba pekee tangu nchi hii iundwe wa IGA ambao uko wazi,” Prof. Kitila Mkumbo- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

‘Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema Bungeni maoni ya watanzania yamesikilizwa na hofu zao na yatazingatiwa kuhakikisha kwamba yatafanyiwa kazi, na hatuna tatizo kwasababu tunatambua kwamba mkataba huu kama ilivyo mikataba mingine, Serikali haijasaini Bibilia wala haijasaini Quran, imesaini Mkataba mikataba yote duniani uwa inarekebishika na kipo kipengele ambacho kinaruhusu marekebisho ambayo ni ibara 22  ambacho kinaruhusu Marekebisho’- Prof. Kitila Mkumbo- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

‘Kwahiyo Serikali haina tatizo na wataalum na watanzania wenye nia njema wanaosema uwekezaji uendelee na baadhi ya vipengele vya kwenye mkataba viangaliwe Serikali itafanyia kazi maoni ya Wananchi waliyoyatoa’- Prof. Kitila Mkumbo- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post