CHANGAMOTO MIRADI YA MAJI KIGOMA KUPATIWA UFUMBUZI



Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Balozi Peter HUYGHEBAERT ambaye ameambatana na Viongozi kutoka Taasisi ya Enabel ya Ubeligiji kwa ajili ya kuzungumzia maswala mbalimbali ya Mashirikiano katika sekta ya Maji kati ya Tanzania na Ubeligiji.

Mazungumzo haya yamefanyika ofisi ndogo za Wizara ya Maji makao makuu ya DAWASA Dar Es Salaam.


Sambamba na hilo pia wamejadili kwa pamoja changamoto kadha wa kadha zinazoikabili miradi ya Maji chini ya Shirika la Enabel linaloshirkiana na Wizara kwa niaba ya Serikali ya Ubelgiji katika sekta ya Maji.


Ikumbukwe tarehe 15-20 mwezi juali,2023 Waziri Aweso alifanya ziara mkoani Kigoma na kubaini changamoto katika miradi ya Kazuramimba, Mkongoro I, Kifura na Kidyama iliyopo katika Mkoa wa Kigoma ambayo inatekelezwa na Taasisi ya hii.

Katika kikao hicho Mhe Waziri pamoja na Mhe Balozi wamekubaliana kushugulikia changamoto hizo zitakazowezesha miradi hiyo kukamilika na kutoa huduma iliyokusudiwa.


Aidha Mhe Waziri Aweso akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng Nadhifa Kemikimba pamoja na Balozi Balozi Peter HUYGHEBAERT wamejadiliana maswala mbalimbali ya kuboresha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Ubelgiji.

Post a Comment

Previous Post Next Post