Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho, leo Jumanne Juni 23, 2026 ameshiriki Mkutano wa Tatu wa Bunge na kupiga kura ya ndiyo kuidhinisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Kupitishwa kwa bajeti hiyo ya Shilingi trilioni 62.33 kunadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha uchumi wa taifa, kuboresha huduma za kijamii na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuinua ustawi wa wananchi.
Bajeti hiyo pia inaweka mkazo katika kuimarisha uwezo wa ulinzi wa taifa kupitia uboreshaji wa mifumo ya kiutendaji, vifaa na rasilimali za kijeshi, hatua itakayoongeza weledi, utayari na ufanisi wa vyombo vya ulinzi katika kulinda mipaka, kudumisha amani na kuhakikisha usalama wa taifa.
