Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Dkt. Jafar Seif, ameshiriki kikao cha Bunge jijini Dodoma na kupiga kura ya ndiyo wakati wa kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/2027.
Bajeti hiyo inalenga kuimarisha huduma za afya, elimu, maji na miundombinu sambamba na kuongeza fursa za ajira na kukuza uchumi jumuishi unaowanufaisha wananchi wote.
Bajeti hiyo pia inaweka mkazo katika kuimarisha sekta ya afya kupitia maboresho ya huduma za tiba, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, pamoja na kuimarisha miundombinu ya afya ili kuongeza ubora na ufanisi wa huduma kwa wananchi na kuchochea maendeleo ya taifa kwa ujumla.
