Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Tajikistan Mhe Ziyozoda Sulaymon ambapo amewasilisha salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuipongeza nchi ya Tajikistan kwa maandalizi ya Mkutano wa umoja wa Mataifa wa Maswala ya Maji.
Waziri Aweso amekutana na Naibu Waziri Mkuu mara baada ya kushriki na kuhutubia Mkutano wa Nne wa Umoja wa Mataifa wa Maji na Maendeleo Endelevu (International Water Decade 2018-2028: Water for Susutainable Development) unaofanyika tarehe 25-28 Mei 2026 jijini Dushanbe nchini Tajikistan.
Katika mkutano ambao Mhe. Aweso, anamwakilisha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tanzania na Tajikistan wameanzisha mazungumzo ya kushirikiana katika Sekta ya Maji ikiwemo uwekezaji kwenye maji na kuimarisha huduma ya maji vijijini na matumizi ya teknolijia sambamba na mikakati ya kujengeana uwezo hususani katika ujenzi wa mabwawa ya kuhifadhi Maji.
