WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Aprili 26, 2026 anazungumza na wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam ambapo amefanya ziara ya kikazi ya siku moja.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara unaofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Msimbazi, Dkt. Mwigulu amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi wa vitendo na mwenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia watanzania kwa kutoa majawabu ya changamoto zinazowakabili.
Aidha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa ofisi zote za umma zipo kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania kwa kutoa majawabu ya kero za wananchi.
Awali Mheshimiwa, Dkt. Mwigulu alikagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mkwajuni lenye urefu wa mita 20 na kimo cha mita 5.5 ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 11.6.
Pia, Mheshimiwa Waziri Mkuu alikagua mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigogo lenye urefu wa mita 50 kimo cha mita 8.9 na barabara unganishi zenye jumla ya urefu wa mita 625 ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 17.7.
