TANZANIA NA MALAWI ZINAENDELEZA USHIRIKIANO WA NISHATI KWA KUIMARISHA USAFIRISHAJI WA MAFUTA


Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nishati na Madini wa Malawi, Mhe. Dkt. Jean Mathanga yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kihistoria baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya nishati hususani usafirishaji wa mafuta.

Kikao hicho kimefanyika leo Machi 25, 2026 katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Ndejembi amesisitiza dhamira ya Tanzania ya kuendelea kushirikiana na Malawi katika kuimarisha sekta ya nishati kwa manufaa ya wananchi wa nchi zote mbili.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini wa Malawi, Mhe Dkt. Jean Mathanga ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuonyesha ushirikiano katika sekta ya nishati.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio, Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati pamoja na wataalamu wa wizara za nchi zote mbili.

Post a Comment

Previous Post Next Post