WANANCHI ILEJE WAISHUKURU SERIKALI UJENZI BARABARA YA ISONGOLE-ISOKO KM 52


Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi  ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja Wilayani humo ambayo imechangia fursa za ajira kwa vijana na wanawake na kuahidi kutoa ushirikiano unaohitajika kwa wakandarasi ili miradi hiyo ilete tija na ufanisi kwa ustawi wa wananchi.

Akizungumza katika ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya wilayani humo Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi kutumia vizuri fursa hizo ili kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

" Miradi hii ya ujenzi wa miundombinu imeleta fedha nyingi hivyo tunakila sababu ya kuishukuru Serikali na kuzilinda kwa kufanya kazi kwa bidii ili kupata matokeo chanya kwa haraka", amesisitiza Mgomi.

Nao wananchi wa Kata za Sange na Isoko wamesema kukamilika kwa ujenzi wa barabara wilayani humo kutakuza biashara ya mazao ya chakula na biashara na kukuza uchumi wa wananchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Naibu Waziri Kasekenya ambae pia ni Mbunge wa Ileje amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuufungua ukanda wa milimani kwa kujenga barabara ya lami na kuahidi kusimamia kikamilifu ujenzi huo ili kufanikisha nia ya Serikali ya kukuza uchumi kwa wananchi katika maeneo yote.

Post a Comment

Previous Post Next Post