DKT. KIJAJI AITAKA TTB KUONGEZA NGUVU KATIKA UTAFITI NA MASOKO


Serikali Kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Tanzania ya Utalii Tanzania kuongeza nguvu katika utafiti na masoko ya bidhaa za Utalii ili kufikia lengo kufikia idadi ya watalii milioni 8 kama ilivyoelekezwa katika ilani ya CCM ya mwaka 2025-2030.

Takwa hilo limetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea Bodi ya Utalii Tanzania Jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana naNaibu Waziri Mhe. Hamad Hassan Chande, Katibu Mkuu Dkt.Hassan Abbas pamoja na Wakurugenzi Kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

"Jambo kubwa ambalo tumeweza kuelekezana ni kuweza kubadilisha mfumo wetu wa kuyafikia masoko kule nje kufikia wateja wetu tunaowalenga kule nje ili waweze kuja ndani ya Taifa letu na tuweze kwenda kwenye lile letu la watalii milioni 8 kwa miaka 5 ijayo".

Pia Waziri Dkt. Kijaji ameitaka Bodi ya Utalii kuboresha bidhaa ambazo wanapeleka sokoni ili watalii wanapokuja waweze kurudi na kuvutia wengine waje jambo ambalo litaongea pato la Taifa.

Katika hatua nyengine Waziri wa Maliasilinna Utalii ameielekeza TTB kuongeza nguvu katika utafiti ili kujua ni vituo gani ambazo havijafika sokoni, viko wapi na kufanya kazi na taasisi zingine ambao ni wamiliki wa maliasili tulizokuwa nazo nchini.

Aidha Dkt. Kijaji amegusia uwepo wa mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) ya mwaka 2027 na kuwataka TTB kutumia fursa ya mashindano hayo kuleta watalii wengi zaidi nchini Tanzania.

Kupitia Mashindano haya tunataka wageni waje kwa wingi kuangalia michezo na wengine waje Tanzania katika msimu hup kwa ajili ya tu ya kutalii kwenye vivutio vyetu tulivyojaaliwa nchini Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post