Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limetoa wito kwa Wafanyakazi wote Nchini kujitokeza kwa wingi siku ya Oktoba 29 kwenda kupiga kura ili kupata Viongozi watakaowaongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo.
Wito huo umetolewa na Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania Cde. Tumaini Peter Nyamhokya alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Arusha leo Alhamisi tarehe 23 Oktoba 2025 lengo likiwa ni kutoa hamasa sambamba na kuwakumbusha wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao hivyo kuwataka Wanafanyakazi kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025 kwenda kupiga kura ili tuweze kuwachagua viongozi watakaojali maslahi ya Wafanyakazi.
“Narejea Kauli mbiu yetu ya Mei Mosi 2025, “Uchaguzi Mkuu wa 2025 utuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki’. Sasa ni wakati wa kwenda kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu yetu ili tuhakikishe mika mitano ijayo mambo yetu yanaendelea kuwa safi. Shime sote tushiriki.Alisisitiza rais wa TUCTA
Katika hatua nyingine rais wa TUCTA ametumia mkutano huo na waandishi wa habari kumshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri na utayari wake kuendelea kutatua changamoto mbalimbali za wafanyakazi na kuzipatia uzito hoja zao zinazowasilisha kwake kisha akataja kwa kifupi machache ambayo Mhe. Rais amewafanyia wafanyakazi katika kipindi cha uongozi wake.
Katika mkutani huo na wana habari Rais wa TUCTA aliambatana na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo la Wafanyakazi Tanzania Cde. Hery Mkunda pamoja na Wanachama kutoka Vyama Shiriki vinavyounda TUCTA waliopo katika Jiji la Arusha na mikoa jirani.
