Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Bara (MNEC) Ndugu Mussa Mwakitinya ameendelea na ziara yake ya kunadi Wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM kwenye mkoa wa Kagera na Jana Ijumaa alikua kwenye Wilaya ya Bukoba Vijijini kumnadi Mgombea Ubunge wa CCM wa Jimbo hilo Dkt. Jasson Rweikiza pamoja na madiwani wa CCM.
Naibu Katibu Mkuu Mwakitinya amefanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye Kata ya Kishogo iliyopo ndani ya Tarafa ya Katerero ambapo ameendelea kuwaomba wananchi kuendelea kuiamini CCM kupitia kwa Mgombea wake wa Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akibainisha takribani Bilioni 80 zilizoletwa Tarafa ya Katerero pekee yake kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo upanuzi Bandari ya Kemondo, Madaraja matatu makubwa na ya kisasa kuanzia Kyanyabasa, Kalebe na Kyetema na mingine mingi iliyotapakaa kila kata.
Aidha, NKM awali asubuhi alifanya Kikao cha ndani na Vijana kutoka Kata zote 29 za Bukoba Vijijini kwenye ukumbi wa MATI uliopo Kata ya Maruku.
Katika hatua nyingine, wakati Naibu Katibu Mkuu anarudi Kata ya Kishogo kwenye ziara ya kampeni alipita pia kuona maendeleo ya ujenzi wa Daraja kubwa la Kisasa la Kalebe linalogharimu Bilioni 9.7 likiunganisha Jimbo zima la Bukoba Vijijini na kukuta Kazi ikiendelea.