DKT. TULIA : MTU WA KAZI NIMEJIANDAA KUFANYA KAZI KUBWA NDANI YA JIMBO JIPYA LA UYOLE


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Tulia Ackson,  leo 05 Oktoba, 2025 amewataka Wananchi Kujiandaa kupokea Maendeleo kwani amejipanga kufanya kazi kubwa ndani ya Jimbo hilo Jipya kwakuwa yeye ni Mtu wa Kazi.

Akizungumza kwenye Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika eneo la Mwakasole Kona Kata ya Isyesye kwaajili ya Kuinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Dkt. Tulia amesema alipoiongoza Mbeya Mjini kwa Mika Mitano amefanikiwa kupeleka Maendeleo mengi kupitia Serikali ya CCM na yeye binafsi kujiongeza kama Mbunge.

Ameeleza kuwa Kupitia Serikali ya CCM Chini ya Mgombea Uraisi Dkt. Samia Suluhu Hassan Baadhi ya Miradi mikubwa ya Kimaendeleo iliyofanyika ni Pamoja na kuanza Ujenzi wa Barabara ya Njia Nne, Uboreshaji Miundombinu ya Afya kwa Kujenga Vitu vya Afya na Zahanati, Ujenzi wa Madarasa na Ukarabati wa Shule Mbalimbali za Msingi na Sekondari, Kuanza utekeleza wa Mradi wa Maji Mto Kiwila utakaomaliza Changamoto ya Upatikanaji wa Maji Mbeya na Maeneo jirani.

Sambamba na hayo Dkt. Tulia amesema kupitia ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025- 2030 yameelezwa Mambo Mengi ya Kimaendeleo yatakayofanyika ndani ya Jimbo la Uyole na Taifa kwa Ujumla ambayo atayasimamia kwajili ya Maendeleo ya wakazi wa Jimbo hilo na ameweka wazi kuwa shuguri nyingine binafsi za Kimaendeleo alizokuwa akizifanya kama vile Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, kuwasaidia wanaoishi kwenye Mazingira Magumu zitaendelea kufanyika kwani amejiandaa kufanya kazi ndani ya Jimbo la Uyole.

Katika hatua nyingine Dkt. Tulia amewataka wakazi wananchi wa Isyesye kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura za heshima Wagombea wa CCM kwa nafasi ya Raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan, Nafasi ya Ubunge Dkt. Tulia Ackson na Madiwani wa CCM 29 Oktoba 2025.

Kampeni za Jimbo la Uyole zinapambwa na kaulimbiu ya "Uyole Kazi" ikilenga Kufanya kazi Kwa Maarifa na Nguvu Zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post