"CHADEMA WAMEAMUA KUSUSA TUSIWAIGE TUKAPIGE KURA - NAPE


"Katiba haitungwi kuwa Katiba ya Uchaguzi, inatungwa kuwa katiba ya maisha ya watu, tukiitunga wakati tunaenda kwenye uchaguzi tutatunga katiba ya uchaguzi. Busara hiyo ndio imekipelekea Chama Cha Mapinduzi kuingiza suala la Katiba mpya kwenye Ilani yake ya uchaguzi na huu ni uungwana wa Mama Samia akasema mengine yote mliyotaka ambayo hayahusiani na Katiba nimewapa, sasa jamaa zangu pamoja na kupewa yote bado wamezira, sasa ukizira sisi tunaendelea na tunachotaka ukizira, zira mwenyewe usisababishe wengine kuzira, zira wewe na wenzako kalale nyumbani, waachie watanzania haki ya kupiga kura tarehe 29 Oktoba.

Kwahiyo yoyote anayeipenda Tanzania, Muumini wa kweli wa demokrasia atakubaliana na mimi kwamba tarehe 29 ukienda kupiga kura unapigia kura mchakato wa katiba mpya ya Tanzania kusimamiwa kwa mujibu wa taratibu na anayepinga hilo abaki nyumbani, anayelitaka hilo twende kwenye vituo vya kupigia kura tarehe 29 tukamalize mambo. Jamaa wale wakati mwingine ukimpa kila kitu anazira, unamwacha pembeni, njaa ikimuuma atarudi mwenyewe na mimi ninaamini waliozira wameamua kuua chama chao wenyewe sasa kama wameamua kuua wenyewe, walikitengeneza wenyewe, wamekiua wenyewe basi watanzania tusizire na anayezira, tarehe 29 twende tukapige kura kwa demokrasia ya Tanzania.

"Tumpigie kura mwanademokrasia wa kweli, muumini wa demokrasia Dkt. Samia Suluhu Hassan."- Nappe Nnauye, Mgombea Ubunge Jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM akimnadi Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 02, 2025 Jijini Arusha kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid.

Post a Comment

Previous Post Next Post