WANANCHI KYERWA WAFUNGUKA UJENZI WA BARA BARA KATA YA MABIRA


Wananchi wa Kata ya Mabira Wilayani  Kyerwa wameipongeza Serikali  kwa kuanza ujenzi wa  Barabara ya Nkwenda-Mabira  kwa kiwango cha lami  ambapo wamedai kuwa mradi wa Barabara  hiyo ukikamilika  wataongezea wateja  wa kununua  mazao yao na kurahisisha usafiri na usafirishaji.

Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 umeweka jiwe la Msingi katika Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.0  katika barabara hiyo  ambayo inatarajia  kukamilika Septemba mwaka huu.

Bw. Ramadhan Robert na Bw. Bosco Gabriel wakazi wa Mabira wamesema wamekuwa wakikutana na athari za vumbi na  mali zao kuchafuka hali inayopekelekea   kukosa soko  hasa mazao kwani yakijaa vumbi ila baada ya ujio wa mradi huo kama wafanyabiashara wamejawa   furaha na kudai kuwa mradi huo ukikamilika uende sambamba na taa za barabarani kwa sababu mji huo umeanza kukukua kwa kasi.

Meneja wa TARURA wilaya ya Kyerwa Mhandisi Yezron Mbasha amesema kuwa mradi huo umegharimu kiasi Cha shilingi Milioni 471.3 ikiwa ni fedha ya serikali inayotokana na tozo za mafuta.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza hadhi  ya mji wa Mabira na kusaidia usafirishaji wa mazao kutoka katika eneo hilo hadi maeneo mengine ya wilaya na Kyerwa na wilaya jirani.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ussi amewataka wananchi kutunza na kulinda Miradi hiyo huku akiipongeza TARURA kwa kutekeleza miradi yenye viwango  na yenye ubora ikiwa ni pamoja kuongeza kasi ya upatikanaji wa barabara za lami katika vijiji na maeneo yanayokua kwa kasi.

Post a Comment

Previous Post Next Post