Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Serikali ya Mwanamke kwa maendeleo endelevu (WSDO) Bi Mary Mwenisongole, Alitembelea shule ya sekondari ya wasichana ya bunge kwa lengo la kutoa elimu ya kujitambua kwa wanafunzi hao ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa program ya SAUTI YA SHANGAZI yenye lengo la kutoa elimu ya kujitambua kwa Mabinti ikiwa na lengo la kuwakumbusha kuhusu safari yao ya mafanikio na uvaaji wa magauni matatu
Katika semina hiyo pamoja na mambo mengine ilitolewa elimu ya uzalendo, kujitambua, hedhi salama na dhana ya uvaaji wa magauni matatu kwa mtoto wa kike. Aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii, kumtanguliza Mungu mbele na kutambua kuwa wao ni Taifa la Leo na kesho na kuyaishi malengo waliyojiwekea kwani inawezekana kuyafikia wakiamua
Pamoja na elimu hiyo waligawa mahitaji ya shule ikiwemo Mabegi ya shule, madaftari, Taulo za kike, Kalamu na Mpira kwa ajili ya michezo.
BINTI JITAMBUE, JIAMINI, JIKUBALI, UNAWEZA
