Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) Dkt. Tulia Ackson, ameendela Kufanya Mikutano yake ya Kampeni kuinadi ilani ya Chama hicho katika kata za Jimbo Jipya la Uyole na kuwahakikishia Wananchi kuwa Barabara za Mitaa zitajengwa kwa Kiwango cha Lami bila kusahau ukamilishaji wa Barabara ya njia Nne inayojengwa Kutoka Uyole hadi Ifisi.
Akizungumza Mbele ya Wananchi wa Kata ya Iduda leo 29 Septemba 2025 Dkt. Tulia amesema katika Kuhakikisha Miundombinu ya Barabara inaboreshwa ndani ya Jimbo hilo CCM imedhamiria Kukamilisha Ujenzi huo unaotumia gharama kubwa na tayari umeshaanza bila kuathiri Ujenzi wa Barabara za Mitaa ya Jimbo la Uyole kwa Kiwango Cha Lami.
Katika hatua nyingine, amesema kwenye sekta ya Elimu ndani ya kata ya Iduda CCM imejenga Madarasa ya Kidato cha Tano na Sita Shule ya Sekondari Iduda pamoja na Miundombinu mingine ikiwemo maabara ili wanafunzi waweze kupata Elimu bora, Pia Changamoto ya Upungufu wa Madawati imemalizika kwa Shule zote za Msingi na Sekondari.
Sambamba na hayo Dkt. Tulia amesema kwenye Sekta ya Afya atahakikisha anamalizia Ujenzi wa Nyumba ya Daktari wa Zahanati ya Iduda ili huduma zipatikane Wakati Wote, Kwenye Sekta ya Maji amewaahidi Wakazi wa iduda Kutoa Maji Kwenye Kisima cha Shule ya Sekondari Iduda ili kuwahudumia huku akiutaja Mradi wa Mto Kiwila kama suluhisho pekee la Changamoto ya upatikanaji wa Maji Jimboni hapo.
Dkt. Tulia amewataka Wananchi wa Jimbo la Uyole na Watanzania Kwa Ujumla ifikapo 29 Oktoba 2025 Kujitokeza Kwa Wingi Kupiga Kura kuchagua Viongozi wanaotokana na CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa CCM ili Waweze kuwaletea Maendeleo ya Kweli
Kampeni za jimbo la Uyole zinapambwa na kaulimbiu ya "Uyole Kazi" ikilenga Kufanya kazi Kwa Maarifa na Nguvu Zaidi.
