USALAMA NI NGUZO YA MAENDELEO TAIFA - DC SHAKA HAMDU SHAKA


Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka leo amehitimisha  na kufunga mafunzo ya wiki miezi 4 ya askari 114  mkupuo wa 20 wa jeshi la Akiba yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya  Msingi Mvumi.

Akizungumza na wahitimu na wananchi waliojitokeza katika sherehe hizo DC Shaka amepongea na kutoa shukrani za dhati kwa JWTZ kupitia Makao Makuu na Kamandi ya Jeshi la Akiba kwa kuratibu mafunzo  kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu na kupelekea wilaya hiyo kuongeza idadi ya askari kila mwaka.

"Mshauri  Jeshi la Akiba  nifikishie Pongezi zangu huko, tunaelewa kuwa Jeshi la Akiba ni nguzo muhimu katika mfumo wa ulinzi wa Taifa letu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua wajibu wa kila raia kulinda uhuru, umoja, na usalama wa nchi yetu"  Shaka.

Amewataka Askari hao mafunzo waliyoyapata yasiishie kwenye kuhitimu bali wakayaishi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku katika kuisaidia jamii na nchi hasa wakati wa matukio muhimu na ya msingi ambayo hugusa uzalendo wa kila mmoja.

"Mkiwa uraiani ndeleeni kuwa mfano wa nidhamu, utiifu na uzalendo katika jamii, mnapoitwa kwa majukumu ya taifa, mjitokeze bila kusita, mkiweka mbele maslahi ya nchi kuliko binafsi "

" Muwe mstari wa mbele katika kusaidia kudhibiti majanga, ulinzi na usalama wa raia, na kushirikiana na vyombo vyengine  vya ulinzi na usalama kwa kutambua viashiria vya uhalifu, kuviripoti na kuvidhibiti"  Shaka

Aliwakumbusha vijana kuwa Taifa letu  liinahitaji wananchi wenye moyo wa kujitoa kama walivyothibitisha wao na kuwa  sehemu ya safu muhimu ya ulinzi wa nchi.

"Morogoro na Wilaya ya Kilosa  zina nafasi kubwa katika uchumi wa nchi kutokana na kilimo na rasilimali nyingine ambapo usalama ni nguzo ya maendeleo, nendeni  mkawe chachu ya kuhakikisha usalama inakuwa ajenda  endelevu kwa nchi yetu" Shaka

Hata hivyo DC Shaka amebainisha kuwa Jeshi la  Akiba ni chelezo la Taifa lipo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inabaki salama, yenye mshikamano, na yenye maendeleo. 

"Hii ndio Tanzania anayoipigania Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wito wangu kwenu nyote muendelee kuwa mabalozi wa amani, mshikamano, na maendeleo katika kila eneo mtakalokuwepo"  Shaka

Post a Comment

Previous Post Next Post