TUCTA YAIPONGEZA SERIKALI KWA MAREKEBISHO YA KIKOKOTOO NA MIFUMO MAFAO YA WATUMISHI


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Tanzania (TUCTA) Hery Mkunda ameeleza ndani ya miaka minne ya Uongozi wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, mageuzi mbalimbali ya kikanuni na kisheria yemefanyika katika kada ya utumishi wa Umma, suala ambalo limeondoa changamotoz vilio na kero mbalimbali na kujenga taswira nzuri ya Wafanyakazi kwa serikali ya Rais Samia.

Mtendaji Mkuu huyo wa TUCTA kwaniaba ya wafanyakazi wa Tanzania ametaja mageuzi hayo kuwa ni pamoja na hatua ya Serikali kuongeza kiwango cha malipo ya mkupuo ya Pensheni kwa Wastaafu kutoka asilimia 33% ya sasa mpaka 40% kwa wafanyakazi waliokuwa walipwa asilimia 50% kabla ya mifuko kuunganishwa na asilimia 35% kwa watumishi ambao walikua wakipokea asilimia 25% kabla mifuko hiyo kuunganishwa na serikali.

Mkunda katika maelezo yake amebainisha kuwa mabadiliko hayo ya kikokotoo hayakuwahusu tu waliostaafu kuanzia Julai 2024 bali wamenufaika wastaafu wote kwa viwango hivyo vipya ikiwemo watumishi 17,068 waliostaafu kuanzia julai 2022 hadi juni 2024 ambao wamelipwa mapunjo yao ya asilimia 7% na wale waliopanda asilimia 33% kwenda asilimia 35% wamelipwa asilimia 2% ambayo walistahili kupata kulingana na mabadiliko yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu.

Mkunda kadhalika ametoa shukrani pia kwa Rais Dkt. Samia kwa kuridhia kurejeshewa michango ya asilimia tano na asilimia kumi ya mifuko ya hifadhi ya Jamii kwa waliokuwa watumishi wa Umma walioondolewa katika utumishi kwenye mchakato wa uhakiki wa vyeti uliofanywa na serikali ya awamu ya tano.

Katika hatua nyingine, TUCTA pia kupitia kwa Katibu Mkuu wake, imetoa pongezi kwa serikali ya Rais Samia kwa kufanya marekebisho kwenye mifumo ya mafao ya utumishi wa umma ambapo kwasasa Mtumishi yeyote anayestaafu ndani ya mwezi mmoja anaanza kupata mafao yake suala ambalo limejenga na kukuza mtazamo chanya wa watumishi wa Umma kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

Previous Post Next Post