Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeshiriki kikamilifu maadhimisho ya wiki ya anwani za makazi iliyoanza leo tarehe 06 mpaka 08 Februari 2025, yaliyoadhimishwa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention centre, 12 Br. ya Jakaya kikweke, 41104 Tambukareli, Dodoma.
(Pichani) ni Watumishi wa TCRA katika banda la maonesho wakiongozwa na Meneja wa Kanda ya Kati , Mhandishi Asajile John (Katikati) aliyemuwakilisha Mkurugenzi mkuu kwenye hafla ya Kilele cha maadhimisho hayo yaliyofungwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa (Mb.).
Timu ya TCRA ya wataalamu ya masuala ya wateja, posta na rasiliamali za mawasiliano na teknolojia ikiongozwa na Bi. Thuwayba Hussein Afisa TEHAMA Mkuu wametoa elimu kuhusu TCRA na nafasi yake katika muundo wa taarifa kamili ya Anwani za Makazi ikiwa ni pamoja na kupanga, kutumia, kutoa na kusimamia rasilimali namba maalum za maeneo zinazojulikana kama Postikodi.
TCRA inaendelea kutoa wito kwa wananchi wote kufahamu na kutumia anwani za makazi pamoja na kuelendea kutunza miundo mbinu yake.