Waziri wa nchi ofisi ya Rais (mipango na uwekezaji) mhe. Prof Kitila Mkumbo ametoa maagizo kwa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kuwalinda wawekezaji hususani wa ndani ya nchi ili wasikwame katika suala la uwekezaji huku akiwaasa pia kuwawezesha pale panapostahili ili kukuza sekta ya uwekezaji nchini
Prof Kitila ametoa maagizo hayo hii leo Jumapili Januari 5, 2025 wakati alipotembelea kiwanda cha (Mati Super brands Ltd) kilichopo mkoani Manyara kinachomilikiwa na mwekezaji mtanzania David Mulokozi ambapo amewaasa TIC,kituo cha uwekezaji Tanzania, Kuwatazama wawekezaji kwa jicho la kipekee na kuhakikisha hawakwami kwa namna yoyote ile katika kufanikisha shughuli zao za kiuwekezaji
"Niwaelekeze TIC wawekezaji kama hawa muwape jicho la pekee uwekezaji wao usikwame hata dakika moja"
Aidha katika hatua nyingine Kitila amewaasa TIC, kuwawezesha wawekezaji kwa namna yoyote ile ili kuhakikisha wanafanikisha uwekezaji wao na kuliingizia taifa kipato huku akihaidi serikali kuhakikisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji nchini na kuahidi kuwasikiliza pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali
"kile ambacho wanachotaka kufanikisha tuwawezeshe wafanikiwe na tuwahaidi sisi kama serikali kuendelea kuwekeza mazingira wezeshi kwa wawekezaji hapa nchini"
Prof Kitila amehitimisha rasmi ziara yake hii leo Januari 5, 2025 mkoani Manyara ambapo ametembelea kiwanda cha uzalishaji bidhaa changamshi(vileo) cha Mati Super brands Ltd kinachomilikiwa na mwekezaji wa ndani David Mulokozi ambapo kitila ametumia nafasi hiyo kumpongeza kwa uwekezaji huo mkubwa na kuahidi serikali kushirikiana naye kwa ukaribu