KWA WASTANI KWA MWEZI TUNALIPA KODI BILLION 1"_MULOKOZI



Mwekezaji wa ndani na mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza bidhaa changamshi (vileo) cha Mati Super brands Ltd  David Mulokozi amesema katika juhudi za kukuza sekta ya uwekezaji nchini  na kuongeza pato la taifa kwa kulipa kodi, kiwanda chake kimepiga hatua katika suala la kulipa kodi huku akibainisha kwa wastani kimefikia kulipa billioni moja kwa mwezi

Ameyasema hayo hii leo Jumapili Januari 5, 2025 wakati akitoa taarifa fupi ya maendelo ya kiwanda hicho mbele ya Waziri wa nchi ofisi ya Rais (mipango na uwekezaji) prof Kitila Mkumbo ambapo amesema kwa miaka mitatu kiwanda hicho kimekuwa kikipiga hatua katika suala la ulipaji kodi ambapo kwa mwaka 2022 wamelipa kodi kiasi cha shilingi billioni 7.7, mwaka 2023 wamelipa shilingi billioni 7.9 huku mwaka 2024 wamelipa shilingi billioni 8

Huku akibainisha makadirio ya kiwanda hicho katika suala la ulipaji kodi kwa mwaka 2025 kufikia shilingi billioni 12 kwa mwaka sawa na shilingi billioni 1 kwa mwezi "kuna ongezeko kubwa pia la kulipa kodi ambayo imeweza kufika wastani wa zaidi ya shilingi billioni moja"amesema Mulokozi

Wakizungumza wafanyakazi wa kiwanda hicho wamesema kuwa kiwanda hicho kimekuwa msaada mkubwa kwao kuwapatia kipato na kusaidia kuendesha familia zao kwa kulipa kodi na hata kulipa ada mashuleni

"Maisha yanaweza kuendelea kupitia ajira tuliyoipata hapa tunaweza kuendesha familia,kusomesha watoto" amesema mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho

Aidha kwa upande wake  Valentine Vedastus kaimu meneja wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kanda ya kaskazini amesema kama TIC wamefurahishwa na uwekezaji wa kiwanda hicho kwani umetoa fursa kubwa kwa vijana huku akihaidi kushirikiana na wawekezaji nchini katika kuhakikisha sekta hiyo inakuwa na mchango mkubwa wa kutoa ajira kwa vijana wengi zaidi

Kiwanda hicho kimetoa ajira kwa vijana wa kitanzania 269 ambao kati yao wafanyakazi 147 ni wakudumu na wafanyakazi 122 ni wa muda

Post a Comment

Previous Post Next Post