Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe Victoria Mwanziva amefanya ziara ya kikazi kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) katika msitu wa hifadhi wa Rondo uliopo katika Wilaya ya Lindi akihamasisha wananchi wa wilaya ya Lindi kujidhatiti na kupambana dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi.
Ziara imejumuisha zoezi la kukagua kitalu cha uoteshaji miche ya miti kinachosimamiwa na TFS, ukaguzi wa shamba la miti Rondo (Halmashauri ya Mtama)
Katika ziara hiyo, Bi Victoria Mwanziva amepokea taarifa ya utekelezaji kutoka kwa mhifadhi mkuu wa shamba la miti Rond; kuwa kitalu hicho kinaotesha jumla ya miche 700000 kwa ajili ya kuotesha shambani na kugawa bure kwa wananchi wa wilaya ya Lindi.
Hili lilifuatiwa na ukaguzi wa shamba la miti Rondo na kujionea shughuli za ufugaji nyuki na upandaji miti- Rondo Plantation Reserve
Aidha, DC Lindi ametembelea Rondo Forest Reserve, hifadhi ya mazingira asilia ya Rondo ambapo mhifadhi mkuu wa msitu- ameelezea fursa zilizopo katika msitu huo ikiwemo utalii ikolojia na uwekezaji wa mahoteli na kambi za kupokelea wageni (tented campsites)
Katika hatua nyingine, DC Lindi amekagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na wakala wa huduma za misitu (TFS) katika vijiji vinavyozunguka msitu wa Rondo.
Miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari mnara ambapo TFS ilitoka Tshs 50,000,000 na mradi mwingine ni upandaji miti ya kivuli na matunda na kivuli katika shule ya sekondari Chiponda.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi amehitimisha ziara hiyo kwa zoezi la Upandaji wa Miche 200 ya miti asilia katika shule ya sekondari Chiponda.
Ziara hiyo ilikuwa na dhamira kuu ya kukagua Shughuli za kikazi za TFS Wilaya ya Lindi na kuhamasisha utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti.