WAZIRI DKT.KIJAJI AWASILI PEMBA KWA ZIARA YA KIKAZI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege Pemba, Zanzibar leo Septemba 23,2024. Kushoto kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis.

Mhe. Dkt. ashatu amewasili Zanzibar kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo kesho Septemba 24,2024 atatembelea miradi mbalimbali inayosimamiwa na kutekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Visiwani Pemba na Unguja ikiwemo Mradi wa kuimarisha Miundombinu ya Fukwe Sipwese, Mkoa wa Kusini Pemba, Mradi wa jamii wa ujenzi wa ngazi Shehia ya Kizimbani, Mkoa wa Kaskazini Pemba pamoja na kutembelea Mradi wa Uhimili wa Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia mifumo ya ikolojia Vijijini (EBARR) Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Post a Comment

Previous Post Next Post