AWESO AMUWEKA PEMBENI MKURUGENZI MAJI TUNDURU,AAGIZA MILIONI 500 KUIMARISHA HALI YA MAJI


Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amemsimaisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji ya Tunduru Christopher Inocent Mbunda kwa kutotekeleza majukumu yake vyema na kuwa na mipango ya kutatua changamoto na kutowajibika ipasavyo kuimarisha hali ya upatikanaji Maji eneo la Tunduru Mjini jimbo la Tunduru Kaskazini.

Akizungumza katika kikao cha ndani na Waheshimiwa Wabunge wa majimbo ya Wilaya ya Tunduru, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Madiwani, kamati ya siasa ya wilaya na watendaji wa Sekta ya Maji mkoa wa Ruvuma na Wilaya Waziri Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Maji Eng Mwajuma Waziri kwa njia ya Simu kuleta Milioni 500 kuimarisha hali ya upatikanaji Maji Tunduru mjini, Kuleta Gari moja na pikipiki kumi ili kuiimarisha mamlaka ya Maji Tunduru.

Aidha Waziri Aweso ameomba apewe kipindi kifupi cha Miezi mitatu na kwa haraka aunde timu ya wataalamu ambayo ataisimamia yeye mwenyewe kuboresha hali ya huduma ya maji Tunduru Mjini.

Post a Comment

Previous Post Next Post