TANZANIA MABINGWA MCHEZO WA GOLI FEASSSA 2024


Timu ya Tanzania katika mchezo wa mpira wa  Goli imeendelea kuonyesha ubabe wake baada ya kutwaa ubingwa mara nne kwenye mashindano ya FEASSSA 2024 yanayofanyika Mji wa Mbale, nchini Uganda.

Mchezo huo ulizikutanisha  timu zenye wanafunzi wenye uoni hafifu na ni moja ya michezo inayoshindaniwa katika mashindano hayo. 

Timu ya Tanzania ambayo ni mabingwa watetezi wa mpira huo tangu mwaka 2021, wametetea ubingwa wao baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 10-0 dhidi ya timu ya Uganda kwenye  mchezo wa fainali uliochezwa Agosti, 25, 2024 katika viwanja vya shule ya Sekondari Bukedea  nchini humo. 

Aidha, wanafunzi Elisha Innocent Musa pamoja Tumsifu lazaro Kitambuli  wameshika nafasi ya kwanza ya wachezaji bora wa mchezo huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post