STAMICO YAINADI VISION 2030: MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI


Shirika  la Madini  la Taifa (STAMICO) limetoa elimu kwa Umma  namna litekeleza Vision 2030 Madini ni Maisha na Utajiri yenye lengo la kufanya utafiti wa madini wa kina kwa asilimia 50 ya nchi nzima ifikapo mwaka 2030.

Hayo yamebainishwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO , Dkt. Venance Mwasse wakati ametembelea Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba Jijini Dar es salaam yaliyoanza Juni 28 na kumalizika Julai 13, 2024.

Mwasse  ameongeza kuwa katika kutekeleza mkakati wa Vision 2030, STAMICO inaendelea  kuboresha miradi yake ukiwemo  mradi wa  uchorongaji, uchimbaji wa madini ya dhahabu na makaa ya mawe, uzalishaji wa nishati mbadala ya Rafiki Briquettes pamoja na   kuboresha mazingira bora kwa wachimbaji mdogo.

Akielezea kuhusu Sekta ya madini kufungamanishwa na sekta nyingine za kiuchumi , Dkt.Mwasse ameeleza kuwa  kwa kuangalia umuhimu wa Nishati safi , STAMICO  imeamua kuzalisha nishati mbadala  ya kupikia ya Rafiki Briquettes iliyotokana na kuongezea thamani mabaki ya makaa ya mawe kwa lengo la  kubeba ajenda ya utunzaji  mazingira .

Naye ,Bi. Bibiana Ndumbaro Afisa Uhusiano kutoka STAMICO  ameongeza kuwa Shirika linaendelea  kutoa ajira  kupitia miradi yake ikiwemo  uchorongaji, uzalishaji wa mkaa mbadala ambapo mpaka sasa zaidi ya vijana wa kitanzania wanashiriki katika kutekeleza  miradi hiyo.

Ndumbaro amefafanua kuwa STAMICO  inaendelea kutanua wigo wa uchimbaji madini wenye uhakika kwa kusaidia kufanya utafiti  wa kina katika mashapo ili kupata taarifa sahihi za kiwango cha madini kilichomo katika maeneo hayo ya uchimbaji hivyo kupunguza athari za kiuchumi kwa wachimbaji  zinazotokana na uchimbaji wa kubahatisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post