Historia imeandikwa uwanja wa Shujaa wa Afrika Nelson Mandela ambapo shujaa wa Taifa letu la Tanzania Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan amepewa zawadi ya kuungwa mkono kwa kishindo na wananchi wa Mkoa wa Rukwa waliojitokeza kwa wingi wakati wote wa Ziara yake.
Kama ilivyokua Mkoa wa Katavi na hapa mwitikio wa Watanzania umekua mkubwa sana, hamasa imetamalaki kwelikweli na kila pande ya mkoa wa Rukwa na Wilaya zake zikiguswa na ajenda ya maendeleo kwa kina na utatuzi wa yote kuwekwa bayana.
Mwitikio wa wana Rukwa katika ziara hakika wametuma ujumbe juu ya Kibali cha kukubalika kwa Rais Samia kwa Watanzania.
Kwa picha ilioonekana leo viwanja vya Nelson Mandela rekodi ya Katavi imevunjwa na hii ni kutokana mwitikio mkubwa wa wananchi wenye mapenzi na mahaba mazito na Rais wao waliomshangilia dakika zote tisini za mchezo, ni wazi wana Rukwa wamepa zawadi na heshima kubwa Rais Samia.
Mageuzi katika sekta ya kilimo kwa kutangaza Bei mpya ya Mahindi, mafanikio Sekta ya Afya na Elimu Rukwa, mafanikio katika ajenda ya kumtua Mama ndoo kichwani na Sekta ya Nishati nk vimeongeza imani kubwa ya wananchi kwake.
Katika hatua nyingine, Mhe Rais Samia asiechoka na anaefikia maeneo yote kama yalivyopangwa katika ratiba ameweza kuyaedendea akiwa na ari, nguvu na morali ametembelea miradi ya kimkakati, kuweka mawe ya msingi, na kuzindua miradi ambayo ni kielelezo cha utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi na ushahidi wa kazi yake kubwa aliofanya katika kipindi kifupi.
Aidha, Akitokea Mkoani Katavi siku ya kwanza cha kustaajabisha ni kwamba wananchi wa Mkoa huu walijipanga maeneo yote ya barabarani kumsubiri Rais wao, kwa hamu na shauku kubwa sana na wameendelea kujitokeza maeneo yote kwa hamasa kubwa alipofika kuzindua miradi naye hakusita kuwasalimu.
Jambo kubwa, la kipekee na muhimu kuliko yote ni ufanisi wa Mhe Rais kutenga muda wa kutosha kusikiliza changamoto za wananchi kupitia wawakilishi wao na kama hiyo haitoshi anakua pia amekwisha kufanya Homework yake anazo changamoto za maeneo haya na ikiwa hazitasemwa yeye anaziibua na kuwa na majawabu yenye vinasaba vya utekelezaji na matumaini.
Ni Bayana Rais Samia amejikita katika takwimu za maendeleo ya kila eneo na anaweka mjadala mezani kwa kila changamoto kupatiwa ufafanuzi, hakuna anachobakiza; ziara ya namna hii ni msingi wa mafanikio ya serikali kwasababu inamaliza na kutoa dira ya maswala yanayowagusa watu moja kwa moja na dira ya maendeleo ya Wilaya hizo na mkoa kwa Ujumla.
Rais Samia katika hotuba zake anaonesha kwamba kwanza ipo timu yake inayofanya research ya kutosha kwa eneo hisika kwasababu anachambua majambo ya maendeleo ya watu kwa undani kabisa na anagusa mambo yote kwa kina hususani maendeleo yanayogusa watu (People Centered Development).
Mwisho, namba hazidanganyi, macho yetu yanaona, maskio yanasikia na akili zetu zinatupa picha ya kuwa ipo wazi kabisa Mhe Rais ametengeneza njia ya mafanikio ya serikali anayoiongoza mapema, ametustaajabisha na kasi na mapokeo ya wananchi kwake, amejenga imani na amani ya mioyo ya anaowaongoza, ameleta matumaini makubwa kwa watu wa chama chake na watanzania wote kwa ujumla na picha halisi ya ziara hizi ni picha ya kukubalika kwa uongozi wake na udhihirisho wa upendo wa Watanzania kwake na mwisho ndio tafsiri halisi ya kuungwa mkono kwake.