Wananchi wa kata ya Ngarenairobi waliopata ajali ya kuunguliwa na nyumba zao wametakiwa kuwa watulivu kwani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuchunguza chanzo cha moto na kuhakikisha inawapatia huduma muhimu ili kuendelea na maisha yao ya utafutaji.
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Siha (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel alipofika katika kata ya Ngarenairobi wilayani Siha mkoa wa Kilimanjaro na kuwafariji wahanga hao huku akiwahakikishia watoto wao wanaendelea na masomo na huduma muhimu kwa wananchi zinaendelea kupatikana
Dkt. Mollel ametoa wito huo leo wakati akielekea katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Roseline kata ya Ndumeti wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza ziara yake Jimboni humo.
Tags
Habari