TCRA KUWATAMBUA WATOA HUDUMA ZA UTANGAZAJI WANAOFANYA VIZURI


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt. Jabiri Bakari amewasisitiza waandishi wa habari na watoa huduma za utangazaji kuzingatia maadili, kanuni na sheria za kutoa huduma hiyo kwani  sekta hiyo ina mchango mkubwa katika kujenga jamii bora na kuleta maendeleo ya jamii na Taifa.

Dkt. Bakari  amesema hayo katika warsha kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Mwanza iliyoandaliwa na TCRA  tarehe 29 Mei, 2924 ili kuwajengea uwezo na kuwakumbusha kanuni za utangazaji na maudhui mtandaoni, kwa lengo la TCRA la kukuza ubunifu na kuwapa nafasi ya kuanzia vijana wasio na ajira rasmi, watumie fursa ya mtandao kujenga jamii bora.

TCRA imeshaanza mchakato wa kuwatambua  watoa huduma za utangazaji, blogs na maudhui mtandaoni wanaofanya vizuri katika kufuata kanuni na ubunifu.

Post a Comment

Previous Post Next Post