WADAU WATAKIWA KUSHIRIKI KATIKA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO


Mkurugenzi Msaidizi huduma za Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais -TAMISEMI Bi. Subisya Kabuje ameishauri jamii kushiriki  katika suala la  malezi na makuzi ya watoto kupitia vituo vya kulelea watoto.

Amesema hayo Aprili 8, 2024 wakati alipotembelea Vituo vya kulelea watoto wadogo vilivyopo Bahi Sokoni na Mundemu  katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

Amesema lengo la Serikali kujenga vituo vya  malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto chini umri wa miaka mitano ni kwa ajli ya kuwapatia watoto huduma za melezi, makuzi ya awali uchangamshi kwa katika maeneo ya Afya, lishe, ujifunzaji wa awali, malezi yenye mwitikio na ulinzi na usalama.

Bi.Kabuje amesema ni vizuri jamii kuwa na ushirikiano na Serikali kuhakikisha vituo hivyo vinakuwa endelelevu kwa jamii, wazazi na walezi kusaidia watoto hasa katika mahitaji muhimu ikiwemo kuchangia suala la upatikani wa chakula katika vituo hivyo kwani husaidia sana katika malezi na makuzi ya watoto.

Naye Mlezi wa kituo cha Bahi Sokoni Witness Omary amesema Serikali iendelee kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa malezi ya mtoto na jukumu la kulea watoto ni jukumu la jamii hivyo ni  vizuri kushirikiana kwa pamoja ili kuwawezesha watoto  kufikia malengo yao.

Post a Comment

Previous Post Next Post