RAIS SAMIA NA RAIS MWINYI WANA IMANI VIJANA


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amesema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhutmri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zaznibar na Mwenyekiti Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi wanaamini Vijana hivyo wasiipoteze Imani yako kwao.

Ndugu Jokate Mwegelo ameyasema hayo wakato anahutumia Maelfu ya Vinaja na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Katika Vijmwanja vya Gymkhana Afisi Kuu ya UVCVM Zanzibar.

"Ndugu zangu Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wanaamini sisi Vijana ndio jeshi la Chama cha Mapinduzi hivyo tusiwaangushe"

Binafsi nawaahidi Ofisi yangu ya Katibu Mkuu wa UVCCM siku zote itakua wazi kwa ajili ya Vijana, kamwe ofisi yangu haitokua kikwazo kwa Vijana kutimiza malenho yao ya kukitumikia Chama cha Mapinduzi, Imani tuliyopewa na Viongozi kamwe hatutaipoteza" alisema Komredi Jokate.

Post a Comment

Previous Post Next Post