Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo (MNEC) amesema Chama cha Mapinduzi kupitia Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi ilishasema itakapofika mwaka 2025 Fomu ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatoka moja tu ambayo ni ya Dkt Samia Suluhu Hassan vile kwa Uapnde wa Zanzibar itatoka ya Dkt Samia Hussein Ali Mwinyi tu, ameyasema hayo leo tarehe 20 Aprili 2024 alipokua anahutubia Maelfu ya Vija kwenye Mapokezi Gymkhana Zanzibar.
"Ndugu Vijana wenzangu, Secretariat ya Chama Cha Mapinduzi katika mapokezi yake ilisema wazi kuwa katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 itatoa fomu MOJA kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye si mwingine bali ni Dkt. Samia Suluhu Hassan, vilevile kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar ni Dkt. Hussein Mwinyi. Nami kwa Niaba ya Viongozi wakuu wa Jumuiya yetu hii ya Vijana niwaeleze kuwa, Jumuiya yetu imepokea msimamo huo na tutazisaka kura zote mtaa kwa mtaa hadi tuhakikishe Viongozi wetu hawa watashinda kwa kishindo".
"Katika kutimiza wajibu wetu kama Viongozi wa UVCCM Taifa tutawapa ushirikiano wa kutosha Viongozi wenzetu pamoja na Wanachama wetu wote wa ngazi zote ili kuhakikisha kuwa tunapata ushindi wa uhakika katika maeneo yetu" amesema Jokate.
