VIJANA TUENDELEE KUJIIMARISHA KIUONGOZI, KISIASA, KIUCHUMI NA KIJAMII" CDE JOKATE


Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwengelo (MNEC) amewasihi Vijana wa Chama cha Mapinduzi kuendelea kujifunza na kujiimarisha kiungozi, Kisiasa,  Kijamii na Kiuchumi ili wawe chachu ya Taifa Sasa na Baadae, ameyasema hayo alipokua anaongea na Maelfu ya Vijana Gymkhana Zanzibar.

"Vijana kila sababu ya kuhakikisha tunajiimarisha katika Nyanja za Kiuongozi, Kisiasa, Kijamii na Kiuchumi ili tuendelee kuwa chachu kwa Taifa letu la sasa na la baadae. Kwani Viongozi wetu wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na maendeleo ya Taifa lake hususani sisi Vijana."

Aidha Komredi Jokate amewasihi Vijana kushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali Mitaa, Vijiji na Vitongoji 2024 kwa kugombea lakini poa kuzisaka kura za Chama cha Mapinduzi na kuwaunga Mkono Vijana wenzao watakaojitokeza kuwania nafasi katika Uchaguzi huo. 

"Vilevile; nitumie jukwaa hili kuwakumbusha kuwa mwaka huu wa 2024 tuna uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji vyake vyote nchi nzima, Nitoe Rai kwa Vijana wenzangu kuhakikisha kuwa tunazisaka kura za CCM katika maeneo yote tuliyopo na kwa kufanya hivi, itatupa nguvu zaidi ya kuendelea na mapambano ya kuhakikisha CCM itaendelea kushika dola hadi kwa vizazi vijavyo." Alisema Komredi Kojate

Post a Comment

Previous Post Next Post