Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Komredi Jokate Urban Mwegelo amesema Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025 umefanyika kwa kishindo lwani Mamno mengi Mazuri ma Makubwa waliyotegemea kuyafanya ndani ya Miaka 5 yametekelezwa ndani ya Miaka 3.
Komredi Jokate ameyasema hayo leo alipokua anahutumia maelfu ya Vijana waliojitokeza katika Mapokezi yake na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Komredi Abdi Mahmoud Abdi tarehe 20 Aprili, 2024 Gymkhana Zaznibar
"Ndugu Vijana wenzangu, sisi sote ni mashahidi wa mambo mazuri na makubwa yaliyofanywa ndani ya nchi yetu. Mambo ambayo tulitegemea yafanyike ndani ya miaka 5 kwa mujibu wa Ilani yetu ya Mwaka 2020 tumeyaona yakitekelezwa kwa kishindo ndani ya Miaka 3 ya Dkt. Samia Suluhu Hassani pamoja na Dkt. Hussein Mwinyi, Huu ni muujiza mkubwa haujawahi kutokea katika Historia ya ujenzi wa Taifa letu".
Tags
Siasa
