Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo ameungana na Wanawake wanaofanyakazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Korea ya Kusini ikiwa ni sehemu ya Kuadhimisha Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani.
Mbibo alikuwa nchini humo kushiriki Mkutano wa Wadau wa Madini Mkakati wa Asia na Afrika ulioandaliwa na Institute of Geoscience and Mineral Resources ( KIGAM) ya nchini humo.
Mbibo ametumia fursa hiyo kutambua nafasi na mchango wa Wanawake katika maendeleo ya nchi.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake hufanyika tarehe 8 Machi ya Kila Mwaka.
Mwaka huu Maadhimisho hayo yamebebwa na Kauli mbinu isemayo Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Jamii